Daktari wa moyo Dkt. Gikonyo atetea Ripoti ya matibabu inayounga mkono Gachagua katika kesi ya kubanduliwa madarakani.

Daktari wa Moyo Daniel Kibuka Gikonyo amefika mbele ya mahakama kwa uchunguzi wa mashahidi baada ya kuwasilisha tamko la kiakili lililounga mkono Makamu wa Rais wa zamani Rigathi Gachagua katika changamoto ya kisheria inayoendelea juu ya mchakato wake wa kumpandisha daraja. Dk. Gikonyo alijitetea kuhusu tathmini yake ya kiafya ya Gachagua, akiambia mahakama kwamba, kwa…

Read More

Turkana yawajengea uwezo maafisa wa rasilimali watu.

Serikali ya Kaunti ya Turkana imewafunza maafisa 50 wa rasilimali watu kuhusu mfumo wa tathmini ya utendakazi wa wafanyakazi, maarufu kama SPAS, katika juhudi za kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Afisa Mkuu wa Utawala na Usimamizi wa Majanga, Marian Lotieng, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa kuimarisha uwezo wa watumishi wa umma…

Read More

Seneti yatilia shaka ushahidi wa matibabu wa Rigathi Gachagua

Seneti imeibua maswali kuhusu ushahidi wa matibabu uliowasilishwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua katika kesi ya kuondolewa kwake mamlakani. Kupitia kwa Karani wa Seneti Jeremiah Nyegenye, Seneti pamoja na Spika Amason Kingi wamehoji uhalali wa stakabadhi za hospitali zilizowasilishwa na daktari wa moyo Daniel Gikonyo. Seneti inasema kuwa rekodi hizo zina utata na hazikuwahi…

Read More

ODM yaanza kujipanga upya kabla ya uchaguzi wa 2027

Chama cha Orange Democratic Movement, ODM, kimeanza mikakati ya ndani ya kujitathmini kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 huku kukionekana wasiwasi kuhusu hatima ya chama hicho bila Raila Odinga kuwania urais. Kupitia tangazo rasmi, ODM imewaalika wanachama wanaotaka kuwania nyadhifa mbalimbali kupitia tiketi ya chama hicho kuwasilisha maombi yao kabla ya mwezi Juni tarehe…

Read More

Alex Davies-Jones Ajiuzulu kupinga Uongozi wa Waziri mkuu Keir Starmer

Serikali ya Uingereza inaendelea kukumbwa na mtikisiko wa kisiasa baada ya naibu waziri katika Wizara ya Sheria, Alex Davies-Jones, kutangaza kujiuzulu kama ishara ya kupinga uongozi wa Waziri Mkuu Keir Starmer. Katika barua aliyomwandikia Starmer, Davies-Jones amesema kuwa “walistahili kufanya juhudi zaidi” na kwa masikitiko makubwa ameamua kuachia wadhifa wake. Aliongeza kuwa hawezi kuendelea kuhudumu…

Read More

WAIGURU ATETEA USHIRIKIANO WAKE NA RUTO

Anne Waiguru ametetea uamuzi wake wa kuendelea kumuunga mkono Rais William Ruto akisema ushirikiano huo unalenga kuhakikisha Kaunti ya Kirinyaga inanufaika zaidi kimaendeleo kutoka serikali kuu. Akizungumza mjini Wang’uru wakati wa uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa maji wa Mwea, Waiguru alisema hakuna serikali ya kaunti inayoweza kufanikisha miradi mikubwa bila kushirikiana na…

Read More

BAJETI YA ULINZI NA NIS YAONGEZWA KWA KIASI KIKUBWA

Wizara ya Ulinzi na Huduma ya Kitaifa kuhusu Ujasusi zimepangiwa zaidi ya Sh310 bilioni katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27, kiwango kinachoweka sekta ya usalama kuwa miongoni mwa zinazopokea fedha nyingi zaidi nchini. Kwa mujibu wa makadirio yaliyowasilishwa bungeni, Wizara ya Ulinzi itapokea Sh250.02 bilioni huku NIS ikipewa Sh58.62 bilioni. Bajeti hiyo ni ya pili…

Read More

TAHADHARI MPYA YA MAFURIKO TANA RIVER

Gavan wa Tana River Dhadho Godhana pamoja na kamishna wa kaunti hiyo,Joseph Mwangi wametoa tahadhari kali kwa wakazi wanaoishi maeneo ya mabondeni na karibu na Mto Tana kuhama mara moja kuelekea maeneo ya juu kutokana na hatari ya mafuriko makubwa yanayotabiriwa katika siku na wiki zijazo. Onyo hilo linajiri huku kina cha maji ya mto…

Read More