World News
Mahakama Yatoa Mwongozo Mpya kwa Kesi za Mahusiano ya Vijana
Mahakama Kuu imeamua kuwa baadhi ya vifungu vya Sheria ya Makosa ya Kujamiiana haviwezi kutumika kuhalalisha mashtaka dhidi ya vijana walio katika mahusiano ya kimapenzi ya hiari bila shuruti na walio karibu kwa umri. Jaji Bahati Mwamuye alisema utekelezaji wa vifungu vya 8, 9 na 11 vya sheria hiyo dhidi ya vijana wanaohusika katika mahusiano…
Kenya Yataka Mafunzo ya afya yawe na mtaala mmoja kupambana na wimbi la wataalamu kuhama nje ya nchi
Wizara ya Afya imetoa wito wa kuoanisha mitaala katika taasisi za mafunzo ya afya nchini huku ikisisitiza umuhimu wa kuimarisha uwekezaji wa pamoja ili kukabiliana na upungufu wa wahudumu wa afya unaochangiwa na wimbi la wataalamu kuhamia mataifa ya nje kutafuta ajira. Akizungumza siku ya Jumatano katika mazungumzo ya ngazi ya juu na Mkurugenzi wa…
Watu wanne waokolewa baada ya bodi kupinduka Lamu
Shirika la msalaba mwekundu linaendelea na operesheni kubwa ya utafutaji na uokoaji kufuatia ajali ya boti iliyopinduka katika eneo la Kwa Bruno Channel, karibu na eneo la LAPSSET Corridor katika kaunti ya Lamu County. Kupitia ukurasa wake wa X, shirika hilo lilithibitisha kuwa watu wanne tayari wameokolewa wakiwa hai kutoka majini na kukimbizwa katika vituo…
Aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua adai kuwa wakati wa uongozi wake Rais Ruto alimuambia kuwa anataka kuwa tajiri zaidi kuliko watangulizi wake.
Kiongozi wa Chama cha Demokrasia kwa Raia (DCP) Rigathi Gachagua amedai kwamba Rais William Ruto mara moja alimtahadharisha kwamba anakusudia kukusanya utajiri zaidi ya baadhi ya familia tajiri zaidi nchini Kenya. Kiongozi wa DCP, ambaye yupo Uingereza kwa ziara ya kisiasa, alidai kuwa wakati alikuwa bado akishiriki urafiki wa dhahabu na Rais, alisema kwamba anapanga…
Zaidi ya watu Elfu kumi na tano (15,000) wameaga dunia kutokana na virusi vya Ebola.
Hatari kutoka mlipuko hatari wa Ebola ni kubwa katika Afrika ya Kati lakini bado ni ndogo kimataifa, Shirika la Afya Duniani jana Jumatano lilisema, likiongeza kuwa virusi hivo huenda vimekuwa vikienea kwa miezi kadhaa. Mlipuko wa homa ya mapafu yenye kuambukiza sana ulitangazwa katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Ijumaa iliyopita. Ebola imewaua…
Hatua za dharura zimeimarishwa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini Kenya.
SSERIKALI ya Kenya imeimarisha hatua za dharura za kukabiliana na Ebola huku ikiweka timu za wataalamu wa afya katika hali ya tahadhari saa 24 kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Uganda. Waziri wa Afya, Aden Duale, alisema serikali imeanzisha mfumo wa kitaifa wa usimamizi wa dharura kupitia…
Daraja la Tana Bridge mjini Garissa kutamatika mwezi wa nane mwaka huu.
Idara inayohusika na ujenzi wa Barabara hapa nchini almarufu KENHA imeweza kufanya ukaguzi wa Daraja mpya inayojengwa katika maeneo ya mororo na kupewa jina la Tana Bridge. Aidha kulingana naye ‘Engineer’ Michael Ngala kutoka KENHA amewahakikishia wananchi kuwa Daraja hiyo ya kisasa itasaidia pakubwa kwa uvukaji kutoka na kuingia katika kaunti ya Garissa. Bwana Ngala…
Arsenal washinda kombe la Ligi kuu ya uingereza mwaka 2025/2026.
Arsenal imepewa rasmi taji la Ligi Kuu kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 22. Wachezaji wa Mikel Arteta bila shaka walikuwa wameshikana na runinga wakitazama na kufuatia mechi kati ya Manchester City wakicheza dhidi ya Bournemouth kwenye Uwanja wa Vitality, wakijua hata kosa dogo lingeliwapa taji lao la ligi lililodumu kwa muda mrefu. Cityzens…
Shirika la Msalaba Mwekundu latoa msaada Kwa waathirika wa mafuriko mjini Garissa.
Shirika la msalaba mwekundu katika kaunti ya Garissa limeweza kutoa msaada kwa waathiriwa wa mafuriko ya maji ambao kwa sasa wanaishi kwenye kambi tofauti tofauti katika kaunti ya garissa. Akizungumza kwenye ugavi wa vyombo hivyo katika kambi ya FTC (farmers training centre) mjini Garissa,msaidizi wa shirika hilo la msalaba mwekundu Daudi Ahmed amehoji kuwa wametoa…
