Ahmed Khalif Kuenziwa Kupitia Uwanja wa Wajir

Uwanja mpya wa Wajir sasa utajulikana kama Ahmed Khalif Wajir Stadium baada ya Rais William Ruto kukubali ombi la viongozi wa eneo hilo la kumuenzi mwanasiasa mashuhuri marehemu Ahmed Mohamed Khalif.

Hatua hiyo ilitangazwa wakati wa sherehe za Madaraka Day katika Kaunti ya Wajir, ambapo viongozi walieleza kuwa marehemu Khalif aliweka historia kwa kuwa mmoja wa viongozi wa kwanza wa eneo hilo kuhudumu katika ngazi ya juu serikalini.

Rais Ruto pia aliahidi miradi zaidi ya maendeleo katika eneo hilo, ikiwemo ujenzi wa chuo kikuu, barabara, nyumba za makazi na kuboresha huduma za afya. Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 10,000 ni miongoni mwa viwanja vinavyojengwa na KDF nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *