Serikali imeeka mikakati ya kukabili Ebola

Serikali ya Kenya imetoa hakikisho kwa wakenya kwamba wizara ya afya iko imara kuhakikisha wananchi wako salama dhidi ya maradhi ya Ebola ambayo yanaendelea kuripotiwa nchini Congo.

Akizungumza wakati wa sherehe za Eid-al-Adha waziri wa afya nchini Aden Duale alisema kuwa raia wote wanaoingia nchini wanakaguliwa katika mipaka ya taifa hili ili kuhakiksiha kuna usalama wa afya.

Duale alisisitiza kuwa wakenya wasiwe na hofu kwani serikali inahakikisha raia wake wako salama dhidi ya maradhi hayo hatari ambayo pia yaliripotiwa nchi jirani ya Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *