Mamia Ya Mateka Wa Boko Haram Waachiwa Huru Nchini Nigeria

Takriban watu 360 waliokuwa wametekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria wameachiliwa huru.

Watu hao walitekwa mwezi Machi mwaka huu katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Jeshi la Nigeria linasema operesheni ya kijasusi iliyotekelezwa na vikosi vya usalama ndiyo iliyowezesha kuokolewa kwa mateka hao.

Hata hivyo, kundi la Borno South Youth Initiative limedai kuwa lilihusika katika kufanikisha kuachiliwa kwao bila masharti, huku likisema idadi ya walioachiliwa ni watu 416.

Visa vya utekaji nyara vinaendelea kuwa changamoto kubwa nchini Nigeria licha ya juhudi za serikali kukabiliana na makundi ya wanamgambo.

Boko Haram liliingia katika historia ya dunia mwaka 2014 baada ya kuwateka zaidi ya wasichana 200 wa shule kutoka kijiji cha Chibok, huku takriban 90 kati yao wakiwa bado hawajajulikana walipo hadi leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *