Mamia Ya Mateka Wa Boko Haram Waachiwa Huru Nchini Nigeria
Takriban watu 360 waliokuwa wametekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria wameachiliwa huru. Watu hao walitekwa mwezi Machi mwaka huu katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi la Nigeria linasema operesheni ya kijasusi iliyotekelezwa na vikosi vya usalama ndiyo iliyowezesha kuokolewa kwa mateka hao. Hata hivyo, kundi la Borno South…
