Viongozi Walalamikia Kuongezeka kwa Makundi ya Wahuni Kisii

Wakazi wa Kaunti ya Kisii wanaitaka serikali kuimarisha usalama na kuchukua hatua kali dhidi ya wanaohusika na vurugu za kisiasa, kufuatia ongezeko la visa vya mashambulizi vinavyodaiwa kufanywa na makundi ya wahuni huku uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 ukikaribia.

Wakazi hao wanasema matukio ya hivi karibuni yamezua hofu kuhusu hali ya usalama katika kaunti hiyo, wakionya kuwa yanaweza kuhatarisha amani na mshikamano wa jamii ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa.

Wito huo umetolewa baada ya Diwani wa Wadi ya Ichuni, Wyclife Siocha maarufu Embande, kushambuliwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana katika mji wa Kisii. Diwani huyo anaripotiwa kuvamiwa na kundi la watu akiwa katika gereji moja mjini humo na kuachwa na majeraha mabaya kabla ya washambuliaji kutoroka.

Tukio hilo ni la hivi punde katika msururu wa mashambulizi ya kisiasa ambayo yamekuwa yakishuhudiwa katika kaunti hiyo katika miezi ya karibuni, hali ambayo imewafanya viongozi na wananchi kutaka wahusika wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *