Naibu Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Christine Kilalo ametoa wito wa kuimarishwa zaidi kwa ushirikiano wa serikali ya kaunti hiyo na serikali ya kitaifa ili kuweza kupambana na changamoto zinazokumba wakaazi pamoja kufanikisha maendeleo.
Kilalo alisema kuwa migogoro ya mashamba, kuimarishwa kwa huduma na kuwaweza wakaazi kimaendeleleo ni baadhi ya maswala ambayo yanastahili kushughulikiwa ili kuboresha maisha yao.
Aliyasema hayo huku wakaazi wengi wa kaunti hiyo wakiendelea kutoa wito kwa serikali hiyo kusuluhisha matatizo ya umiliki wa ardhi kwa kuhakikisha wakaazi wasio na hati miliki za ardhi wanapata vyeti hivyo pamoja na kuimarisha sekta muhumu kama vile afya.
Akizungumza katika shule ya msingi ya Marasi huko Maungu kaunti ndogo ya Voi wakati wa maadhimidho ya sikuku ya Madaraka, naibu gavana huyo pia alielezea kusikitishwa kwake na ongezeko la visa vya utovu wa nidhamu katika tasisi za elimu, pamoja na kuharibiwa kwa mali, na kuwataka wazazi, walezi pamoja na jamii kuwa mstari wa mbele kudumisha nidhamu kwa wanafunzi.
