Ruto Aipa Gor Mahia Changamoto Ya Kutwaa Ubingwa Wa Afrika

Rais William Ruto ameipa Gor Mahia changamoto ya kuiwakilisha vyema taifa la Kenya katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Rais aliwapokea mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Kenya katika Ikulu ya Nairobi Jumapili baada ya kutwaa ubingwa wao wa 22 wa ligi.

Katika hafla hiyo, Rais aliwasifu kwa mafanikio yao huku akiwataka kuweka juhudi zaidi ili kuwania taji la bara Afrika na kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya Kenya.

Aidha, Rais alisema serikali inaendelea kuwekeza katika sekta ya michezo kupitia ujenzi na ukamilishaji wa viwanja 28 vya kisasa vinavyotarajiwa kukamilika ifikapo mwaka ujao.

Kwa kutambua mafanikio yao, kila mchezaji pamoja na maafisa wa benchi la ufundi walitunukiwa shilingi laki moja, huku klabu hiyo ikipokea shilingi milioni kumi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *