Wakulima katika kaunti ya garissa wanaiomba serikali kuu kuingilia kati swala la mafuriko inayoathiri mimea yao mashambani kila mara. aidha wakulima hao wameisuta kampuni ya kengen pamoja na warma kwa kufungulia maji kutoka kwa mabwawa punde tu yanapojaa. itakumbukwa kuwa mashamba kutoka eneo la Mbalambala hadi Ijara yanatumika kwenye shughuli za ukulima,huku baadhi ya wakulima hao wakikadiria hasara inayokisiwa kuwa zaidi ya shiling milioni mia 500, kando na hayo mkulima kwa jina la Mohamed Hassan amehoji kuwa serikali imekuwa ikiwakandamiza tangu mwaka wa 2004 kwa kufungulia maji pasipo kujali madhara yake kwa wananchi. Mohamed aidha amesikitishwa na jinsi hali inavyokwenda kwani hakuna msaada wowote serikali hutoa ili kufidia wakulima waliopoteza mali yao mashambani. kauli yake Maohamed iliungwa mkono na Amina Issa ambaye ni mmoja wa wakulima katika kaunti ya Garissa,huku wakisema kuwa sasa hawatavumilia tena hali hii kutoka kwa wahusika wanaofungulia maji huku wakishikilia kuwa wataelekea mahakamani ili kutafuta njia ya serikali kuwafidia wakulima wote waliopoteza mali yao shambanai.
Aidha kulingana naye Dubei Mohamed ambaye pia ni mkulima ameisuta vikali serikali ya kaunti ya Garissa huku akishikilia kuwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 serikali ya kaunti ya Garissa imewatelekeza wakulima katika kaunti hiyo kwa kutoshughulikia matakwa yao. wakulima hao pia walidokeza serikali ya kaunti ya Garissa kwa kipindi hicho kirefu haijawahi toa msaada wowote kwa wakulima wanaopoteza mazao yao shambani swala ambalo wanaona kuwa serikali hiyo imeamua kuwapa mgongo.
