Tume ya Huduma kwa Walimu, TSC, imekosolewa na wadau wa elimu kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ukosefu wa usawa katika usambazaji wa walimu nchini.
Katika kongamano la elimu mjini Naivasha, wadau walisema baadhi ya shule zina walimu wengi kupita kiasi huku nyingine zikiwa na uhaba mkubwa.
Mwanachama wa Baraza la Chuo Kikuu cha Multimedia, Beatrice Tonui alisema kuna haja ya tathmini ya kitaifa kubaini uwiano wa walimu na wanafunzi katika shule zote.
Katibu katika Wizara ya Elimu Julius Bitok, pia alikiri kuwa kuna changamoto katika usambazaji sawa wa walimu nchini.
