Chama cha ODM, kinakabiliwa na changamoto ya kudumisha ushawishi wake katika eneo la Gusii kutokana na kuongezeka kwa umaarufu wa aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Baadhi ya viongozi wa chama cha ODM, kutoka Kisii na Nyamira tayari wameonyesha kumuunga mkono Matiang’i, huku wengine wakionekana kusitasita kati ya kuunga serikali ya Rais Ruto au kujiunga na upinzani.
Gavana wa Kisii Simba Arati amesema eneo la Gusii litamuunga mkono Matiang’i iwapo atasalia kwenye kinyang’anyiro hadi mwisho.
Kwa upande wake, mwekahazina wa ODM Timothy Bosire, amewataka viongozi wa eneo hilo kuacha mashambulizi dhidi ya Matiang’i na badala yake kumuunga mkono.
