Wakulima wa Chai Walalamikia Ushuru Mpya wa Asilimia 0.8
Wakulima wa majani chai kutoka maeneo mbalimbali nchini wameibua wasiwasi mkubwa kuhusu ushuru wa asilimia 0.8 uliopendekezwa katika Mswada wa Majani Chai, wakisema hatua hiyo itaongeza mzigo kwa wakulima na kudhoofisha sekta hiyo muhimu ya uchumi. Akizungumza katika kaunti ya Kiambu, mwenyekiti wa kiwanda cha majani chai cha Kagwe, William Muroki Githumbi, alisema wakulima hawakuhusishwa…
