Rais Ruto Aanza Ziara Ya Mataifa Ya Ulaya

Rais William Ruto ameondoka nchini kuelekea barani Ulaya kwa ziara rasmi inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Kenya na mataifa ya Ulaya.

Rais aliondoka Jumapili jioni kuelekea Ubelgiji, Norway na Finland.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu, ziara hiyo inalenga kushawishi uwekezaji zaidi nchini Kenya pamoja na kupanua masoko ya bidhaa za Kenya katika mataifa ya Ulaya.

Akiwa nchini Ubelgiji, Rais anatarajiwa kukutana na Mfalme Philippe katika mazungumzo yatakayolenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Aidha, anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Umoja wa Ulaya akiwemo Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya António Costa pamoja na Rais wa Bunge la Ulaya Roberta Metsola.

Serikali ina matumaini kuwa ziara hiyo itafungua fursa mpya za biashara, uwekezaji na ushirikiano wa maendeleo kati ya Kenya na washirika wake wa Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *