Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Colombia zimetajwa kuwa miongoni mwa migogoro ya wakimbizi iliyopuuzwa zaidi duniani, kulingana na Shirika la Norwegian Refugee Council.
Shirika hilo linasema zaidi ya watu milioni tisa wameyakimbia makazi yao ndani ya Sudan tangu kuzuka kwa vita mwaka 2023, huku wengine milioni nne wakikimbilia mataifa jirani.
Aidha, takriban watu milioni 19 wanakabiliwa na njaa kutokana na mzozo huo unaoendelea.
Mkuu wa shirika hilo Jan Egeland amesema dunia haijatoa kipaumbele cha kutosha kwa mgogoro huo licha ya kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu.
Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zaidi ya watu milioni 21 wanahitaji msaada wa kibinadamu huku kiwango cha ufadhili kikiendelea kuwa cha chini.
