Afisa Mkuu wa Nairobi Akamatwa na Mamilioni ya Fedha

Sakata kubwa limeibuka baada ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC, kumkamata Afisa Mkuu wa Mipango ya Miji wa Kaunti ya Nairobi, Patrick Analo Akivaga.

Katika operesheni iliyofanyika nyumbani kwake Syokimau, maafisa wa EACC walidai kupata zaidi ya shilingi milioni 65 taslimu pamoja na nyaraka mbalimbali za mali, hati za ardhi, magari na vifaa vya kielektroniki.

Uchunguzi huo unahusishwa na madai ya utajiri usioelezeka na utoaji wa vibali vya ujenzi vinavyodaiwa kutolewa kinyume cha sheria.

Mkurugenzi Mkuu wa EACC, Abdi Mohamud, amesema mali zilizobainika zinazua maswali kuhusu chanzo chake ikilinganishwa na mapato rasmi ya afisa huyo.

Analo amekuwa akihusishwa na idara ya mipango ya miji kwa miaka kadhaa, lakini amekana kuhusika na vitendo vyovyote vya rushwa.

Kukamatwa kwake kunajiri wakati Nairobi ikiendelea kushuhudia matukio ya majengo kuporomoka, hali ambayo imeibua wasiwasi kuhusu usalama wa majengo na mfumo wa utoaji wa vibali vya ujenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *