Ushindani wa Ugavana Taita Taveta Wapamba Moto

Ushindani wa kisiasa umeanza kushika kasi katika Kaunti ya Taita Taveta huku idadi ya wanaotangaza nia ya kuwania ugavana katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao ikiendelea kuongezeka.

Gavana wa sasa, Andrew Mwadime, pamoja na naibu wake Christine Kilalo, wanawahimiza wakazi kuwapa muhula wa pili ili wakamilishe miradi ya maendeleo waliyoanzisha.

Kaunti hiyo haijawahi kuwa na gavana aliyehudumu kwa mihula miwili. Gavana wa kwanza John Mruttu alishindwa mwaka 2017 na Granton Samboja, ambaye naye aling’olewa mamlakani na Mwadime katika uchaguzi wa mwaka 2022.

Miongoni mwa waliotangaza nia ya kuwania kiti hicho ni aliyekuwa gavana Granton Samboja, Mbunge wa Wundanyi Danson Mwashako, Seneta Jones Mwaruma, Katibu wa Leba Shadrack Mwadime, pamoja na Anderson Mtalaki na John Mwangemi.

Kwa sasa, John Mruttu amehamishia azma yake katika kinyang’anyiro cha useneta huku Gavana Mwadime akionekana kujiandaa kutetea kiti chake kupitia chama cha UDA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *