Ushindani wa Ugavana Taita Taveta Wapamba Moto
Ushindani wa kisiasa umeanza kushika kasi katika Kaunti ya Taita Taveta huku idadi ya wanaotangaza nia ya kuwania ugavana katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao ikiendelea kuongezeka. Gavana wa sasa, Andrew Mwadime, pamoja na naibu wake Christine Kilalo, wanawahimiza wakazi kuwapa muhula wa pili ili wakamilishe miradi ya maendeleo waliyoanzisha. Kaunti hiyo haijawahi kuwa na…
