Idara inayohusika na ujenzi wa Barabara hapa nchini almarufu KENHA imeweza kufanya ukaguzi wa Daraja mpya inayojengwa katika maeneo ya mororo na kupewa jina la Tana Bridge.
Aidha kulingana naye ‘Engineer’ Michael Ngala kutoka KENHA amewahakikishia wananchi
kuwa Daraja hiyo ya kisasa itasaidia pakubwa kwa uvukaji kutoka na kuingia katika kaunti ya Garissa.
Bwana Ngala pia alihoji kuwa Daraja hiyo mpya itadumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 120,huku akisema kuwa Daraja inayotumika kwa sasa au ile ya kitambo muda wake wa kudumu si mrefu zaidi kutokana na miaka ambazo imetumika tangu ilipojengwa.
Aidha Ngala pia amewahakikishia wananchi kuwa ujenzi wa Daraja hilo mpya yaani Tana Bridge inatarajiwa kukamilika mwezi wa nane mwaka huu wa 2026.
Kando na hayo wakaazi wa mtaa wa mororo wamejawa na furaha kwani tangu mradi huo wa
ujenzi wa Daraja mpya umesaidia pakubwa huku wengi wao wakisema kuwa hawajavamiwa
na mafuriko kama hapo awali miaka ya nyuma.
Kulingana naye mchungaji wa kanisa la Fulgospel Church of kenya ilioko mororo Muhubiri
John Mwaura,ameelezea furaha yake kwa mara ya kwanza kanisa hilo halijazama ndani ya
maji huku akisema kuwa miaka za hapo awali kila wakati mafuriko yanapokuja kanisa lake
huwa linazama ndani ya maji.
