Hali ya kesi za Tundu Lissu, Kizza Besigye na Victoire Ingabire

Platform for African Democrats,ambalo ni jukwaa la kisiasa linalowaleta pamoja viongozi wa upinzani, wanaharakati na vyama mbalimbali vya kisiasa barani Afrika, limekosoa matumizi ya mifumo ya mahakama dhidi ya viongozi wa upinzani katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki.

Jukwaa hilo, lilitaja kesi zinazowakabili Tundu Lissu wa nchini Tanzania, Kizza Besigye wa nchini Uganda na Victoire Ingabire wa nchini Rwanda kuwa sehemu ya ukandamizaji wa kisiasa unaolenga kudhoofisha demokrasia.

Katika taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa viongozi wa PAD mjini Stellenbosch nchini Africa kusini, kundi hilo lilisema baadhi ya tawala za Afrika zinatumia mifumo ya sheria kuwafungulia kesi viongozi wa upinzani wanaotaka mageuzi ya kisiasa na uchaguzi huru.

PAD ilieleza wasiwasi kuhusu kesi ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ikidai kuwa imeendelea kwa muda mrefu bila ushahidi wa kutosha huku akizuiwa kupata matibabu anayohitaji baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka 2017.

Kundi hilo pia, lilizungumzia kesi ya Kizza Besigye nchini Uganda pamoja na kukamatwa kwa Victoire Ingabire na wanachama wa chama chake nchini Rwanda, likidai kuwa hatua hizo zinaonyesha kuendelea kwa ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa kisiasa katika eneo hilo.

Aidha, jukwaa hilo la PAD imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushinikiza kusitishwa kwa kesi hizo na kuhakikisha viongozi hao wanapatiwa haki pamoja na matibabu stahiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *