Serikali ya Kaunti ya Turkana imewafunza maafisa 50 wa rasilimali watu kuhusu mfumo wa tathmini ya utendakazi wa wafanyakazi, maarufu kama SPAS, katika juhudi za kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Afisa Mkuu wa Utawala na Usimamizi wa Majanga, Marian Lotieng, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa kuimarisha uwezo wa watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Washiriki wa mafunzo hayo walitoka katika idara mbalimbali za kaunti pamoja na kitengo cha mishahara.
Lotieng, alisema serikali ya kaunti pia inaendelea kuboresha mifumo yake ya kuratibu shughuli za SPAS kwa wafanyakazi wote.
Aidha, mafunzo hayo yaliwawezesha maafisa hao kuelewa mfumo mpya wa GHRIS unaotumia IFMIS katika usimamizi wa wafanyakazi.
