Turkana yawajengea uwezo maafisa wa rasilimali watu.
Serikali ya Kaunti ya Turkana imewafunza maafisa 50 wa rasilimali watu kuhusu mfumo wa tathmini ya utendakazi wa wafanyakazi, maarufu kama SPAS, katika juhudi za kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Afisa Mkuu wa Utawala na Usimamizi wa Majanga, Marian Lotieng, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa kuimarisha uwezo wa watumishi wa umma…
