Skip to content

Kenya na Ufaransa zatia sahihi makubaliano ya ushirikaino

Kenya na Ufaransa zimetia sahihi mikataba ya ushirikiano katika sekta mbalimbali, hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Nairobi.

Akizungmza baada ya kusaini mikataba hiyo rais Dokta William Ruto alisema kuwa Kenya, itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Ufaransa katika sekta mbalimbi kwa manufaa ya nchi zote mbili.

Mikataba iliyosainiwa ni ya sekta ya uchimbaji madini, sekta ya fedha, usafiri wa reli na kawi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Marcon pia alisema wataendelea kuiunga mkono mikataba ambayo imekuwepo na kuongeza ushirikiano katika nyanja mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *