Skip to content

Gavana wa zamani Taita Taveta John Mtuttu awataka wanafunzi kukoma kuchoma shule

Mwenyekiti wa bodi ya shirika la kupeana mikopo kwa wakulima (AFC) John Mruttu amewataka wanafunzi kukoma tabia ya uchomaji wa shule katika kaunti ya Taita Taveta kufuatia visa kadhaa kushuhudiwa siku za hivi karibuni.

Mruttu pia amewataka washika dau mbali mbali ikiwemo wazazi,walimu sawa na viongozi wa dini kuja pamoja na kuangazia suluhu juu ya changamoto hiyo

Wakati huo huo Murutu ambaye ni gavana wa kwanza kaunti ya Taita Taveta ameongeza kuwa changamoto ya uchomaji shule iliwahi kushuhudiwa miaka ya 2013/2014 na ikasuluhishwa kwa njia ya mazungumzo jambo ambalo linafaa wakati huu bila kulaumiana.

Haya yanajiri huku baadhi ya shule ambazo ziliripotiwa kuchomwa zikisalia kufungwa huku wanafunzi wakisubiri tarahe rasmi za kuregelea masomo pamoja na kulipa hasara iliyosababishwa na visa hivyo vya moto.

Shule hizi zilishuhudia visa hivi juma la kwanza shule zilipofunguliwa kwa muhula wa pili wakati ambapo wazazi wengi walikuwa wamelipa karo za muhula huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *