Bunge Lakanusha Madai ya Ushuru Mpya wa Ardhi

Bunge la Kitaifa limefafanua kuwa taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu kuanzishwa kwa ushuru mpya wa kila mwaka kwa ardhi kupitia Mswada wa Fedha wa 2026 ni za uongo na zinapotosha umma.

Kupitia taarifa rasmi, Bunge limesema Mswada wa Fedha wa mwaka 2026 una vifungu 57 na hakuna kifungu chochote kinachohusu kuanzishwa kwa ushuru wa ardhi ya umiliki huru.

Aidha, limekanusha madai kuwa tayari kuna sheria iliyopitishwa au kutiwa saini na Rais William Ruto kuhusu ushuru huo.

Bunge limesisitiza kuwa taarifa hizo zisizo sahihi zimekuwa zikisababisha hofu miongoni mwa wananchi hasa katika kipindi hiki ambapo mjadala kuhusu kodi na gharama ya maisha unaendelea nchini.

Masuala ya ardhi nchini Kenya yameendelea kuwa nyeti kutokana na umuhimu wake katika urithi, uchumi na maisha ya jamii, hali inayofanya taarifa kama hizo kuibua mjadala mkubwa.

Wananchi wametakiwa kupuuza taarifa hizo na kutegemea mawasiliano rasmi kutoka kwa taasisi za serikali kuhusu masuala ya sera na kodi.

Top of Form

Bottom of Form

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *