Marsabit: Mwalimu kizimbani kwa tuhuma za kunajisi

Mwalimu mmoja Jumatatu alifikishwa katika mahakama ya Marsabit kwa madai ya kumnajisi mwanafunzi wa umri wa miaka 14.

Denis Kipkoech Chepkwony mwenye umri wa miaka 29 alikabiliwa na shataka la kumnajisi mwanafunzi huyo kati ya tarehe 5 na tarehe 18 mwezi April mwaka huu wa 2026 katika eneo la Kargi, kaunti ya Marsabit.

Mshtakiwa pia anakabiliwa na shtaka la pili la kutenda tendo la aibu la kumpapasa sehemu za siri msichana huyo wa umri mdogo.

Hata hivyo Chepkwony akiwa mbele ya hakimu mkaazi wa mahakama ya Marsabit, Edward Oboge alikanusha mashtaka yote dhidi yake.

Hakimu Oboge aliagiza mshukiwa kuzuiliwa katika kituo cha polisi huku akisubiri mwelekeo wa kesi.

Mahakama pia inasubiri ripoti kutoka kwa afisi ya kuchunguza tabia ili kutathmini iwapo mshukiwa anaweza kuachiliwa kwa dhamana au la.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 8 mwezi wa Juni mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *