Wahudumu wa matatu mjini Garissa hii leo wameweza kulemaza shughuli za usafri hii ni
baada ya wahudumuhao kuungana na wenzao kote nchini kwenye mgomo wa vyombo vya usafri kutokana na ongezeko la bei ya mafuta.
Aidha mapema asubuhi ya leo makumi ya wasafri mjini madogo walilazimika kutumia
pikipiki kuendekazini huku weingine wakilazimikakutembeakwa miguuhadimjini
Garissa.
Hata hivyo wahudumu hao wa gamama sako wa magari ya uchukuzi kutoka madogo Kwenda Garissawameapa kuwa hawatarejelea shughuli za usafri hadi pale serikali itakapopunguza
bei ya mafuta.
Kulingana naye Mohamed Hajir ambaye ni dereva wa matatu mjini Garissaamedokeza kuwa
amesikitshwa pakubwa na bei ya ongozeko la mafuta kwa kipindi cha muda mfupi.
Hajir amesema kuwa wao kama wahudumu wa magari ya umma wanapita kipindi kigumu
kutoka kwa wasafri ambao hawako tayari kulipia nauli mpya kando na ile ya zamani.
Kwa sasa nauli mpya ya matatu kutoka mjini madogoo KwendaGarissani shillingi 40 huku
nauli ya awali ikiwa ni shillingi 30 jambo ambalo baadhi ya abiria wamelazimika kukubali
shingo upande.
Kwa upande wake Swaleambaye ni mmoja wa wahudumu hao wa matatu alichora taswira
kamili jinsi mambo yalivyo kwenye sekta hiyo,Huku akisema kuwa kila siku muhudumu wa
matatu hupata takribani shillingi elfu 6,000ambapo hapo anafaa kumlipa mwenye gari yeye mwenyewe na pia dereva n ahatapia gari lenyewe likipata matatzo hela hizo tu ndizo
hutumika kwenye ukarabat wake
Mgomo huo pia umewaathiri wasafri wengi ambao wanaelekea mjini Nairobi huku mabasi
ya usafri vilevile yakikosekana.
Maandamano mjini Garissa
