Kiongozi wa chama cha DCP, Rigathi Gachagua, ameikosoa vikali sera za uchumi na ajira za serikali, akidai kuwa makato yanayoendelea yameongeza mzigo kwa wafanyakazi nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya soko la ajira ya mwaka 2026, Gachagua alisema makato kama PAYE, SHA, NSSF pamoja na ushuru wa nyumba yamepunguza kwa kiwango kikubwa kipato halisi cha wafanyakazi.
Aidha, alitoa wito wa kuanzishwa kwa mfumo mbadala wa kuwatetea wafanyakazi, akidai kuwa vyama vya sasa havijatekeleza wajibu wake ipasavyo.
Pia alimkosoa Katibu Mkuu wa COTU, Francis Atwoli, akimtuhumu kushindwa kuisimamia ipasavyo ajenda ya wafanyakazi.
Kwa upande wake, Fazul Mohamed alionya kuwa ongezeko la makato bila nyongeza ya mishahara limezidisha shinikizo la maisha kwa wafanyakazi wengi, akisema hali hiyo imeifanya mishahara kupoteza maana yake kwa wengi.
Kiongozi wa chama cha DCP, Rigathi Gachagua, ameikosoa vikali
