Skip to content

Mlipuko wa Ebola Waongezeka Mashariki mwa DRC

Kulingana na taarifa za hivi karibuni kutoka Africa Centres for Disease Control and Prevention, idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola katika taifa la Democratic Republic of the Congo imeongezeka hadi watu 80, huku takribani visa 246 vikishukiwa kuripotiwa katika jimbo la Ituri mashariki mwa nchi hiyo.

Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Mongwalu, Rwampara na Bunia, ambayo ni maeneo yenye shughuli kubwa za uchimbaji wa dhahabu na usafiri wa watu wengi, hali inayoongeza hatari ya kusambaa kwa ugonjwa huo.

Aidha, Africa CDC imeanza uratibu wa kikanda kwa kushirikiana na Uganda na South Sudan ili kuimarisha uchunguzi wa mipakani na kudhibiti maambukizi ya kuvuka mipaka.

Taifa la Uganda tayari imeripoti kisa kimoja kilichoingizwa kutoka DRC ambapo mgonjwa alifariki mjini Kampala.

Awali ilidhaniwa kuwa vifo vilikuwa 65, lakini taarifa mpya kutoka wizara ya afya ya DRC imethibitisha ongezeko hilo hadi 80.

Ugonjwa huu, unasemekana kusababishwa na aina ya Bundibugyo ya virusi vya Ebola, ambayo ni nadra kuliko aina ya Zaire, na kwa sasa hakuna tiba kamili iliyothibitishwa, ingawa huduma za kusaidia wagonjwa huongeza nafasi ya kupona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *