Skip to content

Daraja la Tana Bridge mjini Garissa kutamatika mwezi wa nane mwaka huu.

Idara inayohusika na ujenzi wa Barabara hapa nchini almarufu KENHA imeweza kufanya ukaguzi wa Daraja mpya inayojengwa katika maeneo ya mororo na kupewa jina la Tana Bridge.

Aidha kulingana naye ‘Engineer’ Michael Ngala kutoka KENHA amewahakikishia wananchi

kuwa Daraja hiyo ya kisasa itasaidia pakubwa kwa uvukaji kutoka na kuingia katika kaunti ya Garissa.

Bwana Ngala pia alihoji kuwa Daraja hiyo mpya itadumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 120,huku akisema kuwa Daraja inayotumika kwa sasa au ile ya kitambo muda wake wa kudumu si mrefu zaidi kutokana  na miaka ambazo imetumika tangu ilipojengwa.

Aidha Ngala pia amewahakikishia wananchi kuwa ujenzi wa Daraja hilo mpya yaani Tana Bridge inatarajiwa kukamilika mwezi wa nane mwaka huu wa 2026.

Kando na hayo wakaazi wa mtaa wa mororo wamejawa na furaha kwani tangu mradi huo wa

ujenzi wa Daraja mpya umesaidia pakubwa huku wengi wao wakisema kuwa hawajavamiwa

na mafuriko kama hapo awali miaka ya nyuma.

Kulingana naye mchungaji wa kanisa la Fulgospel Church of kenya ilioko mororo Muhubiri

John Mwaura,ameelezea furaha yake kwa mara ya kwanza kanisa hilo halijazama ndani ya

maji huku akisema kuwa miaka za hapo awali kila wakati mafuriko yanapokuja kanisa lake

huwa linazama ndani ya maji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *