Skip to content

Shirika la Msalaba Mwekundu latoa msaada Kwa waathirika wa mafuriko mjini Garissa.

Shirika la msalaba mwekundu katika kaunti ya Garissa limeweza kutoa msaada kwa waathiriwa wa mafuriko ya maji ambao kwa sasa wanaishi kwenye kambi tofauti tofauti katika kaunti ya garissa.

Akizungumza kwenye ugavi wa vyombo hivyo katika kambi ya FTC (farmers training centre) mjini Garissa,msaidizi wa shirika hilo la msalaba mwekundu Daudi Ahmed amehoji kuwa wametoa msaada kwa watu 1000.

Aidha shirika hilo liliwapa waathiriwa hao hema,blanketi,mikeka,mitungi ya maji,dawa ya maji,sabuni,neti miongoni mwa vitu vingine.

Kando na hayo mwaathiriwa kwa jina Abubakar Hamisi Barisa aliridhishwa na jinsi usajili wa walioathiriwa na mafuriko ulivyofanywa na shirika hilo la msalaba mwendu kwani ameamini kuwa kulikuwa na uwazi tangu mwanzo hadi kufikia ugavi wa vitu walivyopewa kutoka kwa shirika hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *