Skip to content

Alex Davies-Jones Ajiuzulu kupinga Uongozi wa Waziri mkuu Keir Starmer

Serikali ya Uingereza inaendelea kukumbwa na mtikisiko wa kisiasa baada ya naibu waziri katika Wizara ya Sheria, Alex Davies-Jones, kutangaza kujiuzulu kama ishara ya kupinga uongozi wa Waziri Mkuu Keir Starmer.

Katika barua aliyomwandikia Starmer, Davies-Jones amesema kuwa “walistahili kufanya juhudi zaidi” na kwa masikitiko makubwa ameamua kuachia wadhifa wake.

Aliongeza kuwa hawezi kuendelea kuhudumu katika mazingira ambayo hayalingani na matarajio yake ya uwajibikaji.

Kujiuzulu kwake kunamfanya kuwa afisa wa tatu wa serikali kuondoka ndani ya muda mfupi, baada ya naibu waziri mwingine pia kutangaza kujiuzulu kwa sababu zinazotajwa kuwa kutoridhishwa na uongozi wa Starmer.

Jess Phillips ambaye pia alitangaza kujiuzulu, amesema hawezi kuendelea kuhudumu chini ya uongozi wa sasa kwa sababu “haoni mabadiliko aliyoyatarajia.”

Kujiuzulu kwa manaibu mawaziri hao kunatokea wakati ambapo idadi inayoongezeka ya wabunge wa chama cha Labour wanamtaka Starmer ajiuzulu, wakisema ameshindwa kuonyesha mwelekeo thabiti wa kisera na kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *