Ruto Aagiza Matatu Kuendelea Kutumia Grafiti Na Sanaa
Rais William Ruto, ameagiza Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA) kuruhusu wahudumu wa matatu kuendelea kutumia michoro ya graffiti na sanaa kwenye magari ya uchukuzi wa umma. Akizungumza kutoka Ikulu ya Mombasa, Rais alisema serikali itahakikisha mazingira mazuri kwa waendeshaji wa matatu kuendelea kuonyesha ubunifu na sanaa kwenye magari yao huku wakizingatia…
