Skip to content

Jaji Mkuu Martha Koome amesisitiza umuhimu wa uthabiti

Jaji Mkuu Martha Koome amesisitiza umuhimu wa uthabiti, maadili na misingi imara ya maisha, akieleza kuwa mafanikio yake yametokana na kuvumilia changamoto na kujifunza kupitia misukosuko ya maisha.
Akizungumza katika kipindi cha She Means Business, Koome, alirejelea simulizi zilizomo kwenye kitabu chake Courting Courage, akibainisha kuwa safari yake imejengwa juu ya malezi yenye misingi ya nidhamu, imani na kuthamini elimu.
Alimtaja mama yake kama mhimili mkuu wa maadili hayo, akisema kuwa mafunzo aliyopata utotoni ndiyo yaliyoendelea kumwelekeza katika maamuzi yake ya maisha na taaluma.
Aidha,alieleza kuwa kusawazisha majukumu ya kifamilia na kitaaluma ni changamoto halisi inayohitaji dhamira, mipango thabiti na uwepo wa mifumo ya msaada.
Koome pia, alikumbuka kushindwa kwake katika jaribio la kwanza la kuwania wadhifa wa Naibu Jaji Mkuu, akisisitiza kuwa tukio hilo halikumrudisha nyuma bali lilimjengea uthabiti na ari mpya ya kusonga mbele.
Kwa upande wa masuala ya kitaifa, alitoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya ufisadi, akisisitiza kuwa uwajibikaji ni jukumu la kila mmoja katika jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *