Skip to content

Raia wa Kenya wanaoishi Afrika Kusini

Raia wa Kenya wanaoishi Afrika Kusini wametakiwa kuchukua tahadhari zaidi kufuatia maandamano yanayoripotiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo, yanayowalenga wageni.
Ubalozi wa Kenya nchini humo umewasihi Wakenya kuepuka maeneo ya mikusanyiko ya maandamano, kubeba vitambulisho vyao muda wote, na kufuata maelekezo ya vyombo vya usalama.
Aidha, wametakiwa kuripoti matukio yoyote ya dharura kwa mamlaka husika au ubalozi kwa msaada zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *