ODM yaanza kujipanga upya kabla ya uchaguzi wa 2027

Chama cha Orange Democratic Movement, ODM, kimeanza mikakati ya ndani ya kujitathmini kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 huku kukionekana wasiwasi kuhusu hatima ya chama hicho bila Raila Odinga kuwania urais. Kupitia tangazo rasmi, ODM imewaalika wanachama wanaotaka kuwania nyadhifa mbalimbali kupitia tiketi ya chama hicho kuwasilisha maombi yao kabla ya mwezi Juni tarehe…

Read More

Alex Davies-Jones Ajiuzulu kupinga Uongozi wa Waziri mkuu Keir Starmer

Serikali ya Uingereza inaendelea kukumbwa na mtikisiko wa kisiasa baada ya naibu waziri katika Wizara ya Sheria, Alex Davies-Jones, kutangaza kujiuzulu kama ishara ya kupinga uongozi wa Waziri Mkuu Keir Starmer. Katika barua aliyomwandikia Starmer, Davies-Jones amesema kuwa “walistahili kufanya juhudi zaidi” na kwa masikitiko makubwa ameamua kuachia wadhifa wake. Aliongeza kuwa hawezi kuendelea kuhudumu…

Read More

WAIGURU ATETEA USHIRIKIANO WAKE NA RUTO

Anne Waiguru ametetea uamuzi wake wa kuendelea kumuunga mkono Rais William Ruto akisema ushirikiano huo unalenga kuhakikisha Kaunti ya Kirinyaga inanufaika zaidi kimaendeleo kutoka serikali kuu. Akizungumza mjini Wang’uru wakati wa uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa maji wa Mwea, Waiguru alisema hakuna serikali ya kaunti inayoweza kufanikisha miradi mikubwa bila kushirikiana na…

Read More

BAJETI YA ULINZI NA NIS YAONGEZWA KWA KIASI KIKUBWA

Wizara ya Ulinzi na Huduma ya Kitaifa kuhusu Ujasusi zimepangiwa zaidi ya Sh310 bilioni katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27, kiwango kinachoweka sekta ya usalama kuwa miongoni mwa zinazopokea fedha nyingi zaidi nchini. Kwa mujibu wa makadirio yaliyowasilishwa bungeni, Wizara ya Ulinzi itapokea Sh250.02 bilioni huku NIS ikipewa Sh58.62 bilioni. Bajeti hiyo ni ya pili…

Read More

TAHADHARI MPYA YA MAFURIKO TANA RIVER

Gavan wa Tana River Dhadho Godhana pamoja na kamishna wa kaunti hiyo,Joseph Mwangi wametoa tahadhari kali kwa wakazi wanaoishi maeneo ya mabondeni na karibu na Mto Tana kuhama mara moja kuelekea maeneo ya juu kutokana na hatari ya mafuriko makubwa yanayotabiriwa katika siku na wiki zijazo. Onyo hilo linajiri huku kina cha maji ya mto…

Read More

Bunge la seneti lapendekeza sheria ya kuzikinga serikali za kaunti kutokana na upungu wa fedha

Kamati ya Seneti kuhusu fedha na bajeti imewasilisha mapendekezo ya marekebisho ya muswada wa ugavi wa mapato wa mwaka 2026 ambayo yanaitaka serikali ya kitaifa kugharamia peke yake upungufu wowote wa mapato utakaojitokeza katika mwaka wa kifedha wa 2026/2027. Marekebisho hayo, yaliyoorodheshwa katika ajenda ya Seneti kabla ya kikao cha Jumanne, yanapendekeza kifungu kipya kinachoeleza…

Read More

TSC YAPIGWA DARUBINI KUHUSU MGAWO WA WALIMU

Tume ya Huduma kwa Walimu, TSC, imekosolewa na wadau wa elimu kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ukosefu wa usawa katika usambazaji wa walimu nchini. Katika kongamano la elimu mjini Naivasha, wadau walisema baadhi ya shule zina walimu wengi kupita kiasi huku nyingine zikiwa na uhaba mkubwa. Mwanachama wa Baraza la Chuo Kikuu cha Multimedia, Beatrice Tonui…

Read More