Maelfu ya wakenya mapema Jumatatu walilazimika kutembea kuelekea kazini, huku wengine wakisalia nyumbani kwa kukosa usafiri, baada ya kuanza rasmi kwa mgomo unaopinga ongezeko kubwa la bei ya mafuta, huku ikikadiriwa kuwa gharama ya maisha pia huenda ikaongezeka.
Naye waziri wa hazina ya kiaifa John Mbadi mapema Jumatatu alisema mgomo huo haukustahili akisema serikali tayari imebeba sehemu kubwa ya gharama za ongezeko hilo lililosababishwa na vita kati ya Marekani na Iran.
Mbadi alikubali kuwa bei ya juu ya mafuta imewaumiza Wakenya na inaweza kuathiri vibaya uchumi kama vile mfumuko wa bei, viwango vya riba, akiba ya fedha za kigeni na thamani ya shilingi.
