Skip to content

Wakulima mjini Garissa waomba msaada kutoka kwa serikali kuu kuhusiana na mafuriko.

Wakulima katika kaunti ya garissa wanaiomba serikali kuu kuingilia kati swala la mafuriko inayoathiri mimea yao mashambani kila mara. aidha wakulima hao wameisuta kampuni ya kengen pamoja na warma kwa kufungulia maji kutoka kwa mabwawa punde tu yanapojaa. itakumbukwa kuwa mashamba kutoka eneo la Mbalambala hadi Ijara yanatumika kwenye shughuli za ukulima,huku baadhi ya wakulima…

Read More

Alex Davies-Jones Ajiuzulu kupinga Uongozi wa Waziri mkuu Keir Starmer

Serikali ya Uingereza inaendelea kukumbwa na mtikisiko wa kisiasa baada ya naibu waziri katika Wizara ya Sheria, Alex Davies-Jones, kutangaza kujiuzulu kama ishara ya kupinga uongozi wa Waziri Mkuu Keir Starmer. Katika barua aliyomwandikia Starmer, Davies-Jones amesema kuwa “walistahili kufanya juhudi zaidi” na kwa masikitiko makubwa ameamua kuachia wadhifa wake. Aliongeza kuwa hawezi kuendelea kuhudumu…

Read More

Jaji Mkuu Martha Koome amesisitiza umuhimu wa uthabiti

Jaji Mkuu Martha Koome amesisitiza umuhimu wa uthabiti, maadili na misingi imara ya maisha, akieleza kuwa mafanikio yake yametokana na kuvumilia changamoto na kujifunza kupitia misukosuko ya maisha.Akizungumza katika kipindi cha She Means Business, Koome, alirejelea simulizi zilizomo kwenye kitabu chake Courting Courage, akibainisha kuwa safari yake imejengwa juu ya malezi yenye misingi ya nidhamu,…

Read More

WAIGURU ATETEA USHIRIKIANO WAKE NA RUTO

Anne Waiguru ametetea uamuzi wake wa kuendelea kumuunga mkono Rais William Ruto akisema ushirikiano huo unalenga kuhakikisha Kaunti ya Kirinyaga inanufaika zaidi kimaendeleo kutoka serikali kuu. Akizungumza mjini Wang’uru wakati wa uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa maji wa Mwea, Waiguru alisema hakuna serikali ya kaunti inayoweza kufanikisha miradi mikubwa bila kushirikiana na…

Read More

Rais Ruto awakosoa wapinzani kuhusiana na swala la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Rais William Ruto amejibu wakosoaji wa utawala wake kuhusu jinsi wanavyoshughulikia mgogoro wa mafuta unaoendelea, akiwashutumu wapinzani wa kisiasa kwa kufaidika na mateso ya Wakenya kwa faida ya kisiasa badala ya kutoa suluhisho za vitendo. Akizungumza wakati wa hotuba ya moja kwa moja kutoka Ikulu jijini Mombasa siku ya leo Ijumaa, Ruto alilinda hatua za…

Read More

Gachagua ataja mpango wa uagizaji mafuta kuwa “ulaghai”

Kiongozi wa chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua, ameutaja mpango wa serikali kwa serikali (G-to-G) wa uagizaji mafuta kuwa “ulaghai”, akiishutumu serikali ya Rais William Ruto, pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kwa kuwaumiza Wakenya kupitia ongezeko la bei ya mafuta. Akizungumza kabla ya kuondoka kuelekea United Kingdom, Gachagua alisema mzozo wa…

Read More

Usafiri wa umma walemazwa katika miji mikuu na sehemu tofauti nchini, kufuatia mgomo wa magari ya uchukuzi kulalamikia ongezeko kubwa la bei za mafuta ya Dizeli na Petroli

Maelfu ya wakenya mapema Jumatatu walilazimika kutembea kuelekea kazini, huku wengine wakisalia nyumbani kwa kukosa usafiri, baada ya kuanza rasmi kwa mgomo unaopinga ongezeko kubwa la bei ya mafuta, huku ikikadiriwa kuwa gharama ya maisha pia huenda ikaongezeka. Naye waziri wa hazina ya kiaifa John Mbadi mapema Jumatatu alisema mgomo huo haukustahili akisema serikali tayari…

Read More