SifaFm

Untitled-3

Mwandishi: Geoffrey Otieno

Mkulima wa samaki akikanyaga pampu ya maji

Katika kaunti ya Marsabit, ambako ukame na jua kali vimekuwa sehemu ya maisha ya kila siku, jambo la kushangaza linaibuka, ufugaji wa samaki unaleta mageuzi!

Kupitia ufadhili wa miradi ya mabadiliko ya tabianchi, msaada kutoka kwa Idara ya UvuviShirika la Mpango wa Chakula Duniani (World Food Program) na vikundi vya vijana wa eneo hilo, jamii za North Horr, Saku, Moyale na maeneo mengine sasa wanakumbatia ufugaji wa samaki kama suluhisho jipya dhidi ya njaa, umasikini na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Kutoka mabwawa ya udongo hadi maji yaliyojaa tilapia, mradi huu hauwalishi familia tu bali unajenga ustahimilivu na kuleta matumaini mapya katika eneo lililoonekana halifai kwa ufugaji wa samaki.

Ungependa kujua jinsi samaki wanavyoishi mahali ambapo zamani kulikuwa na mifugo?

 Tazama video hii ya kusisimua kutoka Sifa FM Marsabit naye Susan Mbodze ushuhudie jinsi matumaini yanavyochipuka hata jangwani.

Verified by MonsterInsights