SifaFm

Untitled-3

Hatimaye maafisa wakuu 13 kutoka kaunti ya Taita Taveta walioandikiwa barua na bunge la kaunti hiyo kufika mbele yake ili kuelezea kuhusiana na ubadhirifu wa shilingi milioni nne fedha za hafla ya ukumbusho wa vita vya kwanza vya dunia walifika mbele bungeni.

Maafisa hao waliongozwa na mawaziri wa elimu Gloria Monikombo na mwenzake wa vijana,michezo na utamaduni Shedrack Mutungi.

Kikao hicho kilifanyika wiki moja baada ya kikao cha hapo awali kuhairishwa kutokana na wafanyikazi wanne waliotumwa kwa likizo ya lazima na gavana wa kaunti hiyo Andrew Mwadime kukosa kufika katika vikao hivyo.

Kamati ya bunge ikiongozwa na naibu spika wa bunge hilo Anselm Mwadime ilitaka kujua kutoka kwa mkuu wa wafanyikazi Pamphil Mwakio sababu ya wanne hao kukosa vikao vya awali huku wakielezea masikitiko yao kwa maafisa hao wakuu kudharau mwaliko huo.

Vikao hivyo sasa vitaendelea rasmi Jumanne wiki ijayo ambapo maafisa hao watatarajiwa kueleza wanachokifahamu kuhusu ubadhirifu wa shilingi milioni nne pesa za hafla ya makumbusho ya vita vya kwanza vya dunia katika kaunti hii.

Verified by MonsterInsights